Hii ni Akademia ya mafunzo na malezi ya Afrika ambayo inajishughulisha kusahilisha mafunzo, kusambaza elimu, kuleta karibu masomo ya sharia, kupanua ufahamu na kuelezea utamaduni wa kiislamu na lugha ya kiarabu kupitia njia nyepesi na yenye kuvutia.
MAONO YETU:
Tunataka Akademia yetu iwe ni mlango wa kielektroniki wenye kuongoza katika kusahilisha katika kujifunza uislamu na lugha ya kiarabu miongoni mwa wazungumzaji lugha ya Kiswahili.
UJUMBE WETU
Akademia yetu inafanya bidii kusambaza masomo ya Kislamu na lugha ya kiarabu miongoni mwa wazungumzaji wa lugha za Kiafrika za msingi kupitia uwanja wa kielektroniki ikitumia wataalamu mahiri, teknolojia mahususi, silabasi madhubuti, uongozi wa kielimu na malezi unaojitambua kupitia mpango kamili na njia ya kati na kati iliyo tayari kusikiliza maoni, mazingira ya kielimu yenye kuhamasisha na utumiaji bora wa teknolojia na utendaji kazi mzuri wa kitaasisi
MALENGO:
WALENGWA:
UMUHIMU WA LUGHA YA KISWAHILI:
Lugha ya Kiswahili ina wazungumzaji wapatao au wanaozidi milioni 200, ni lugha inayo sambaa kwa kasi mashariki ya Afrika na ni moja miongoni mwa lugha kumi zinazoenea zaidi ulimwenguni.
Lugha hii inazungumzwa na watu wengi katika Afrika mashariki, vilevile kuna juhudi kubwa zinazolenga kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya mawasiliano katika Bara la Afrika. Katika kongamano la mwisho la maraisi wanachama wa muungano wa Afrika ilikubalika kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi miongoni mwa nchi za muungano, vilevile kwenye mwaka 2019 lugha ya Kiswahili iliibuka kuwa lugha ya kiafrika pekee inayo tambulika na muungano wa Maendeleo kaskazini mwa Afrika, pia huku jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inajiandaa kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi nchini mwake.
MAENEO MUHIMU YA LUGHA YA KISWAHILI:
Kiswahili na lahaja zake inasambaa kuanzia Somalia mpaka Msumbiji, na kupitia sehemu za magharibi ya jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, nazo ni kama zifuatazo:
1.Tanzania 2. Kenya 3. Uganda 4. Msumbiji
5. Burundi 6. Kongo 7.Malawi 8. Somalia
9. Komoro 10. Madagaska