Mpango wa mafunzo ya mbali kwa Muislamu mpya anayezungumza Kiswahili, unaolenga kumfundisha majukumu muhimu ya dini, jinsi ya kuishi kwa mujibu wa Uislamu, na jinsi dini hii inavyoleta athari chanya katika maisha yake, roho yake, furaha yake, na elimu yake. Lengo ni kumwezesha kumwabudu Mwenyezi Mungu kwa elimu na upeo sahihi, na kumwandaa kuwa mlinganizi wa dini ya Mwenyezi Mungu.
* Kuelewa na kutekeleza nguzo za Imani na Uislamu kwa usahihi.
* Kutekeleza ibada za msingi kwa mujibu wa Sunna ya Mtume ﷺ.
* Kutumia sheria za Kiislamu (fiqhi) katika maisha yake ya kila siku.
* Kujipamba na maadili ya Kiislamu katika maisha yake binafsi na ya kijamii.
* Kushiriki kwa ufanisi katika jamii ya Kiislamu na kueneza Uislamu kwa wasio Waislamu.
1- Cheti cha kumaliza programu.
2- Usajili bure katika diploma ya Akademia ya Kiislamu ya Afrika.
3- Cheti cha kujiunga na moja ya vituo vya Kiislamu.
4- Zawadi kumi za fedha kwa wanafunzi kumi bora.
* Vyeti vinavyotambulika: kila mwanafunzi atapata cheti kinachotambulika kutoka kwa akademia.
Nchi | Jina la Mshindi | Zawadi | Daraja | Nafasi |
---|---|---|---|---|
Tanzania | RASHID MOHAMED HAMISI | 200,000 za Kitanzania | 100% | Wakwanza |
Kenya | سالم براسا | 180,000 za Kitanzania | 100% | Wapili |
Kenya | أوكتي آدم سكوى | 150,000 za Kitanzania | 100% | Watatu |
Kenya | Muhammed Maero Namati | 120,000 za Kitanzania | 100% | Wanne |
Kenya | ISRAI ABDALLAH JUMA | 100,000 za Kitanzania | 100% | Watano |